Miaka 30 ya Lionel Messi na rekodi zake 30 alizotegeneza katika ulimwengu wa soka.

Muktasari:

Nyota huyo wa Argentina anatajwa kuwa ni moja wa wachezaji bora wa wakati wote katika historia ya soka.

Barcelona, Hispania. Lionel Messi ametimiza miaka 30 na katika kipindi hicho amefanya kila kitu katika ulimwengu wa soka.

Nyota huyo wa Argentina anatajwa kuwa ni moja wa wachezaji bora wa wakati wote katika historia ya soka.

Alianza kucheza soka la kulipwa rasmini 2004 akiwa na klabu yake Barcelona.

Messi ametwaa ubingwa wa La Liga mara nane, Ligi ya Mabingwa mara nne, Kombe la Mfalme (4), Kombe la Dunia la Klabu la Fifa (3), Uefa Super (3) na Hispania Super Cup (6).

Katika kusherekea miaka 30 ya nyota huyo, hizi hapa ni rekodi 30 alizotegeneza hadi sasa.

1. Ballon d’Or — 5

Messi ametwaa tuzo hiyo 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015 na kumfanya kuwa juu ya nyota wote, lakini ni Ronaldo pekee anayetaraji kuifikia rekodi hiyo kama atashinda 2018.

2. Ni mchezaji pekee aliyefunga mabao zaidi ya 40 katika misimu nane mfululizo

Ndiyo ni msimu wa 2008-09 pekee aliofunga mabao 38, na kushidwa kufikia magoli 40. Tangu wakati huo amekuwa na rekodi ya kufunga mabao 47, 53, 73, 60, 41, 58, 41 na 54 kwa msimu.

3. Ni mchezaji pekee aliyefunga katika mashindano sita tofauti ya klabu katika msimu umoja mara mbili

Messi alifunga katika Hispania Super Cup, La Liga, Uefa Super Cup, Champions League, Kombe la Mfalme na Kombe la Dunia la Klabu la Fifa katika mwaka 2011 na 2015.

4. Ni mchezaji aliyeingia mara nyingi katika tatu bora ya Ballon d’Or top ikiwa ni mara10

Tangu 2007, Messi amekuwa akiingia katika tatu bora ya tuzo hiyo kubwa katika medali ya soka.

5. Aliingia katika rekodi duniani 'Guiness World Record' akifunga amefunga mabao 91 ndani ya mwaka moja

Messi aliweka rekodi hiyo kwa kufunga mabao hayo 2012.

6. Ni mchezaji pekee aliyefunga katika mashindano matatu ya Kombe la Dunia la Klabu la Fifa 2009, 2011 na 2015

Unatakiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa mara tatu ili kufikia rekodi ya Messi.

 

7. Mchezaji aliyefunga mechi nyingi za ligi ikiwa ni mechi 21.

Messi alifunga mabao 33, katika mechi hizo alizocheza mwaka 2013.

 

8. Ni mchezaji wa kwanza kuifunga kila timu katika msimu moja wa ligi.

Alifunga kila mechi ya La Liga katika msimu huo 2012/13.

 

9. Ni mchezaji aliyetwaa mara nyingi tuzo ya mpira dhahabu mara mbili katika Kombe la Dunia la Klabu la Fifa

Alifanya hivyo mwaka 2009 na 2011, lakini mabao matano katika mechi mbili aliyofunga Luis Suarez ndiyo yaliyomnyima Messi asichukue tuzo hiyo 2015.

 

10. Ni mchezaji pekee aliyefunga zaidi ya mabao 60 katika msimu mwili mfululizo.

 

Alifanya hivyo msimu wa 2011-12 (mabao 73) na 2012-13 (mabao 60).

11 . Ni mchezaji kwanza kufikisha mabao 300 katika ligi tano kubwa Ulaya alipofunga mabao 334.

Messi sasa amefunga mabao 349 akiwa na umri miaka 30.

 

12. Mchezaji mdogo zaidi kufikisha idadi ya mechi 100 za Ligi ya Mabingwa

Kwa sasa amecheza mechi 115.

 

13. Mchezaji mdogo zaidi aliyefunga mabao zaidi ya 44 akiwa katika klabu moja Ulaya.

Alipokuwa na miaka 27, alifunga mabao 300 na sasa amefunga magoli zaidi ya 500.

 

14. Mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa msimu 50

Alifikia rekodi hiyo msimu wa 2011-12.

15. Mchezaji aliyefunga idadi kubwa katika klabu yake kwa msimu ilikuwa magoli 73

Alifanya hivyo 2011-12.

 

16. Mchezaji aliyeweka ya kufunga mbao mengi kwa mwaka moja ni  79 ni mwaka 2012.

17. Ni mchezaji pekee aliyefunga magoli katika miji 23 katika mashindano mbalimbali Ulaya.

 

18. Ni mcheaji wa kwanza katika La Liga kufunga mabao mawili katika mechi 100.

 

19. Mfungaji bora wa muda wote wa Barcelona akiwa amefunga mabao 535

 

20. Mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa mpira ya adhabu Barcelona katika 27

 

21. Mchezaji aliyefunga mabao matatu kwa mechi moja 'hat-tricks' kwa Barcelona mara26

 

22. Ni mchezaji aliyetegeneza mabao mengi katika La Liga zikiwa na pasi135 za mwisho

 

23. Ni mchezaji bora kwa wastani wa kufunga mabao La Liga kwa msimu (akiwa na wastani wa mechi 20) 1.44

 

Messi alifunga mabao 46 katika mechi 32 msimu wa 2012-13.

24. Mchezaji kijana zaidi aliyefunga mabao 250 katika La Liga akiwa na miaka 27, lakini sasa anakaribia kufunga  mabao 400.

 

25. Mchezaji wa kwanza wa Barcelona kufunga zaidi ya mabao 30 katika ligi ndani ya misimu miwili.

Messi alifanya hivyo katika mwaka 2009-10 na 2012-13.

 

26. Mchezaji wa kwanza wa Barcelona kufunga zaidi ya mabao 50 kwa msimu.

Amefanya hivyo katika misimu mitano mfululizo.

 

27. Mchezaji wa kwanza wa Argentina kufunga bao dhidi ya mataifa yote yanayoshiriki mashindani ya Copa Amerika chini ya shirikisho la CONMEBOL

 

28. Ni kinara wa ufungaji Argentina amefunga mabao 58

Messi ameivunja rekodi ya Gabriel Batistuta aliyefunga magoli 54.

 

29. Mchezaji kijana zaidi wa Argentina kufunga katika Kombe la Dunia akiwa na miaka18 na siku 357.

Messi alifunga katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Serbia and Montenegro katika Kombe la Dunia 2006.

30. Mchezaji mdogo zaidi katika historia ya CONMEBOL kufikisha idadi ya mechi100, akiwa na miaka 27 na siku361.

Sasa anaiwakilisha nchi yake ikiwa ni mechi 118.