Kipa wa Liverpool ajitwisha zigo la kupoteza mchezo

Kiev, Ukraine. Kipa wa Liverpool, Loris Karius amelaumiwa na mashabiki wa timu hiyo baada ya kutoa kuruhusu kufungwa mabao ya kizembe la kwanza na lile la tatu.
Hata hivyo, mlinda mlango huyo aliwaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana na mabao hayo ya kizembe aliyoruhusu kutinga wavuni.
Kipa huyo alisema kwamba kwa sasa hajisikii vyema kutokana na kuwasababishia  maumivu ya moyo mashabiki wa timu yake kwa kuzamisha mabao 3-1.
Aliongeza kuwa amekuwa chanzo  kwa timu yake kupoteza mchezo muhimu na kuwaomba radhi tena mashabiki wa klabu hiyo.
Aliwaomba pia uongozi mzima wa klabu hiyo kwa makosa ya kibanadamu ambayo aliyafanya wakati akiwa uwanjani, huku akisema kuwa ndiye aliyewaangusha hadi kupoteza mchezo huo.
Mashabiki wa klabu hiyo walimnyoonyea kidole kipa huyo kutokana na kutokuwa makini uwanjani, huku wakimrushia maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.