Mashabiki AS Roma mbaroni England

Muktasari:

Shabiki wa Liverpool mwenye miaka 53, alishambuliwa kwa kupigwa ngumi na idadi kubwa ya mashabiki wa AS Roma.

LONDON, ENGLAND. MASHABIKI tisa wa AS Roma wamekamatwa kwa kosa la kumshambulia shabiki wa Liverpool.

Shabiki wa Liverpool mwenye miaka 53, alishambuliwa kwa kupigwa ngumi na idadi kubwa ya mashabiki wa AS Roma.

Liverpool ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Anfield ilishinda mabao 5-2 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi usiku.

Tukio hilo lilitokea nje ya klabu ya usiku ya Albert na shabiki huyo aliwahishwa hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa baada ya kuumia vibaya.

Taarifa ya polisi inasema shabiki huyo ana hali mbaya kutokana na majeraha aliyopata katika sehemu mbalimbali za mwili.

Polisi wamesema washambuliaji hao wameshikiwa kwa makosa tofauti ikiwemo unywaji wa pombe kupita kiasi na shambulio la kuzuru mwisho.

Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), limeshitushwa na tikio hilo na limetaka kuchukuliwa kwa wahusika.

“Uefa imeshitushwa na tukio hili, tunasubiri taarifa ya ripoti kamili kabla ya kuchukua hatua muhimu kwa utovu mkubwa wa nidhamu,”ilisema sehemu ya taarifa ya shirikisho hilo.