Marcelo kitanzini kwa kukwepa kodi Hispania

Muktasari:

Hata hivyo, mkaguzi wa hesabu wa Real Madrid tayari ameshaandaa malalamiko kuhusu suala hilo ambapo inaonyesha kuwa Marcelo hakuwa na deni tangu mwaka wa fedha 2013.

Hispania. Nyota wa Real Madrid, Marcelo (29) anatuhumiwa na mashataka ya kukepa kodi nchini Hispania inayofikia takribani Pauni 435,000.
Hata hivyo, mkaguzi wa hesabu wa Real Madrid tayari ameshaandaa malalamiko kuhusu suala hilo ambapo inaonyesha kuwa Marcelo hakuwa na deni tangu mwaka wa fedha 2013.
Marcelo amejiunga na Real Madrid tangu mwaka 2007 akishinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika malalamiko ya Real Madrid yanaeleza kwamba Marcelo aliingia makubaliano kwa mwaka 2011, 2012 na 2013 ambayo hayakuhusisha mapato yatokano na haki za matangazo ya picha.