Manuel Neuer apewa unahodha Bayern Munich

Muktasari:

Kipa huyo atakiongoza kikosi hicho kuanzia msimu huu wa mwaka 2017/18 na kuendelea.

Ujerumani. Uongozi wa Bayern Munich umemtangaza Manuel Neuer (31) kuwa nahodha mpya baada ya kustaafu Philipp Lahm.

Kipa huyo atakiongoza kikosi hicho kuanzia msimu huu wa mwaka 2017/18 na kuendelea.

Rais wa klabu hiyo, Karl-Heinz Rummenigge aliyemtangaza nahodha mpya, alisema anaamini mchezaji huyo anaweza kuimudu kazi hiyo kutokana na uzoefu wake klabuni hapo.