Manchester United inatiririka mabao Kombe la Carabao

Muktasari:

Mabao ya Manchester United yaliwekwa wavuni na Marcus Rashford (2), Jesse Lingard na Anthony Martial.

England. Kikosi cha kocha mwenye mbwembwe nyingi, Jose Mourinho kimeiadhibu mabao 4-1 timu ya Burton kwenye mechi ya Kombe la Carabao jana Jumatano.
Mabao ya Manchester United yaliwekwa wavuni na Marcus Rashford (2), Jesse Lingard na Anthony Martial.
Mkali wa mabao Romelo Rukaku hakufanikiwa kutikisha nyavu kwenye mchezo huo ambao Manchester United ilidhihirisha kuwa msimu huu inarudisha heshima yake ya miaka iliyopita.