Man United yatajiwa bei ya Boateng

Muktasari:

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anajulikana kuwa anasaka mlinzi wa kati huku akiendelea kuongea na mlinzi wa Tottenham, Toby Alderweireld, lakini pia inasemekena kuwa ameonyesha nia kwa Boateng.

MANCHESTER United imetajiwa bei ya mlinzi wa Bayern Munich, Jerome Boateng kuwa ni Pauni 50 milioni wakati huu wakionyesha nia ya kumchukua staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani katika dirisha hili la uhamisho.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anajulikana kuwa anasaka mlinzi wa kati huku akiendelea kuongea na mlinzi wa Tottenham, Toby Alderweireld, lakini pia inasemekena kuwa ameonyesha nia kwa Boateng.

Hivi majuzi Bayern walitangaza kwamba wapo tayari kumuuza staa huyo mwenye asili ya Ghana kwa bei mwafaka huku mwenyewe akikaririwa akidai kwamba yupo tayari kusaka changamoto mpya kwingineko.