Man United yanuka fedha mbaya

Muktasari:

Miamba hiyo ya England imefanikiwa kuwapiku Real katika klabu 20 zilizoingiza mapato makubwa zaidi

London, England. Manchester United imeipiku Real Madrid kwa kuwa klabu taji zaidi duniani baada ya kupata mapato mengi zaidi ya barani Ulaya.
Pamoja na kushindwa kucheza Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, Man United imefanikiwa kuwapiku mabingwa wa Ulaya, Real Madrid na kuwa kinara katika ligi ya fedha iliyotolewa na Deloitte.
Baada ya kumsajili Alexis Sanchez kutoka kwa Arsenal, klabu hiyo imetegeneza mapato makubwa kuliko wapinzani wake katika ligi kubwa tano Ulaya.
Katika orodha hiyo wapinzani wa Man United katika mbio za ubingwa England wameingia katika 10 bora ambao ni Man City, Arsenal, Chelsea na Liverpool.
Pia, katika orodha hiyo timu nyingi za England zilizoingia katika 20 bora ni Tottenham, Southampton, Everton na West Ham hiyo yote ni kutokana na mkataba wa haki za TV wanazopata klabu hizo.
Manchester City imekuwa na mafanikio kwa kuongeza pato lake kwa miezi 12 iliyopita yakipanda kutoka pauni 392.6milioni hadi pauni453.5m  na kuwafanya kuingia katika nne bora.
Paris Saint-Germain imeporomoka hadi nafasi ya saba na kupitwa na Arsenal, pamoja na mwaka huu kuvunja rekodi ya uhamisho ya pauni195milioni ya kumsajili Neymar kutoka Barcelona.
Hata hivyo, orodha hiyo haijumuishi fedha ya uhamisho, na kama ngekuwa hivyo basi PSG na Barcelona wangekuwa mbali zaidi.