Man United kutesti mitambo kwa Club America

Muktasari:

  • Wakati United ikiendelea na maandalizi ya mechi hizo, Luke Shaw ameendelea kupambana na hali yake mazoezini ili kuhakikisha anabaki Man United.

Manchester United inajiandaa kwa mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Club America  ya Marekani ikiwa ni mechi ya maandalizi ya Ligi Kuu England.
Wakati United ikiendelea na maandalizi ya mechi hizo, Luke Shaw ameendelea kupambana na hali yake mazoezini ili kuhakikisha anabaki Man United.
Man United inatarajiwa kucheza mechi tano za kirafiki kabla ya kuanza msimu mpya England. Mchezo wake wa kwanza wa kirafiki utapigwa Ijumaa Julai 20 itapokutana na Club America.
Kikosi cha Mourinho kilifaya mazoezi yake kwenye  Chuo Kikuu cha Califonia ambapo Mourinho alitumia muda mwingi kukitazama kikosi chake, huku kila mchezaji akipambana kumshawishi  kocha huyo ili kujihakikishia namba.
Man United ilitua Marekani Jumapili iliyopita na inatarajiwa kutupa karata yake ya kwanza keshokutwa Ijumaa kwenye mchezo huo wa kirafiki utakaopigwa Uwanja wa Chuo Kikuu cha Phoenix unaofahamika Glendale.