Beki Stones kuwakosa Man Utd, Spurs

Muktasari:

Beki huyo wa England alipata maumivi ya misuri wakati wa mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu England dhidi ya Leicester City.

London, England. Kikosi cha Pep Guardiola kimepata pigo katika safu ya ulinzi baada ya beki wake John Stones kulazimika kukaa nje kwa wiki sita.
Beki huyo wa England alipata maumivi ya misuri wakati wa mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu England dhidi ya Leicester City.
Akizungumzia mechi yake ya leo ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Feyenoord, kocha Guardiola alisema: "Mwezi wote wa (Desemba) atakuwa nje.
"Ni matumaini yangu atakuwa amepona vizuri zaidi mwishoni mwa Januari.
"Tunao Manga na Vincent na Nico pamoja na Kyle, Danilo na Fernandinho wote wapo vizuri. Mendy pia nafikiri anaweza kucheza nafasi hiyo."
Stones atakosa mechi 11, zikiwamo mechi mbili kubwa dhidi ya Manchester United na Tottenham Spurs.
Katika mchezo wa Jumamosi walioshinda 2-0, Stones alitolewa dakika 31 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Eliaquim Mangala.