Man City yaenda kucheza mechi kitalii

Tuesday December 5 2017

 

Kikosi cha Manchester City kitasafiri kuifuta Shakhatar Donestsk katika mchezo wa Kundi F utakaopiga kesho Jumatano huku wachezaji hao ni kama wakitalii kutokana na timu hiyo kutangulia kufuzu hatua ya 16 bora.
Licha ya timu hizo mbili vinara kwenye kundi F kukutana mchezo wa kesho, nafasi ya pili inapewa zaidi Shakhtar ambayo inashuka dimbani huku ikiwa na pointi 9 kibindoni.
Mchezo mwingine wa kundi hilo utazikutanisha Feyenoord na Napoli ambazo matokeo mazuri ya Napoli yanaweza kuifanya kufikisha pointi 9 huku akisikilizia mechi ya City na Shakhtar.
Dua mbaya za Napoli wanazielekeza kwa Shakhtar kwamba ipoteze mchezo wake dhidi ya Manchester City ili klabu hiyo ya Italia ipate nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora.