Majigambo yashika kasi mpambano wa McGregor vs Mayweather Agosti 26

Friday July 14 2017

 

Marekani. Tambo za mabondia Conor McGregor na Floyd Mayweather ndiyo habari kubwa Marekani kwenye tasnia ya masumbwi nchini humo.

Kwa mara ya pili tena mabondia hao walikutana ndani ya wiki hii kwa ajili ya kupima uzito ili kujiandaa na pambano lao la Agosti 26.

Mashabiki wa mchezo huo walimiminika kwenye ukumbi wa mikutano na waandishi wa habari kusikiliza majigambo na tambo za mabondia hao maarufu duniani.

Mabondia hao walitunishiana misuli na kurushiana tena maneno ya kejeli huku kila mtu akionyesha kwamba ataibuka mshindi kwenye mchezo wao unaosubiriwa kwa hamu.