Mahrez ashusha mshahara kuivuta AS Roma

Muktasari:

Kocha wa Leicester City, Craig Shakespeare alisema Jumanne iliyopita kwamba klabu hiyo bado haijapokea ofa rasmi inayomhusu staa huyo wa kimataifa wa Algeria, ambaye alitangaza mwishoni mwa msimu uliopita kwamba anataka kuihama huko King Power.

London, England. Riyad Mahrez ameripotiwa kwamba yupo tayari kupunguza mshahara wake ili tu ajiunge na AS Roma ya Italia, lakini bado anasubiriwa ofa rasmi ipelekwe kwenye klabu yake ya Leicester City.