Mahrez aanza kwa kipigo Man City

Muktasari:

Katika mchezo huo wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi mbalimbali barani Ulaya, bao pekee la Dortmund lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Mario Gotze.

Chicago, Marekani. Riyad Mahrez ameanza maisha mpya yake katika kikosi cha Pep Guardiola kwa kipigo Manchester City ikilala bao 1-0 kutoka kwa Borussia Dortmund katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Chicago.
Katika mchezo huo wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi mbalimbali barani Ulaya, bao pekee la Dortmund lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Mario Gotze.
Katika mchezo huo Mahrez akiwa na jezi ya Manchester City alifanikiwa kuonyesha kiwango cha juu huku mpira wake wa adhabu ukiokolewa kwa ustadi mkubwa na kipa Dortmund.
Swali kubwa katika mchezo huo ni kuwa wachezaji watano walioanza katika kikosi cha Man City, Jason Denayer, Aleks Zinchenko, Jack Harrison, Lukas Nmecha na Brahim Diaz watakuwa katika klabu nyingi mwisho wa Agosti.
Wengi waliocheza ni watoto, ukiacha Mahrez na Claudio Bravo pamoja na Eric Garcia beki wa zamani wa Barcelona walifanikiwa kuonyesha kiwango bora.