Chelsea akili yote kwa Liverpool

Muktasari:

Timu hizo zitakutana mwishoni mwa wiki hii katika muendelezo wa Ligi Kuu England

LONDON, ENGLAND. Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameanza kulia ratiba ngumu inayoikabili timu yake inawapa unafuu wapinzani wao Liverpool ambao watakumbana nao Jumamosi ijayo.
Chelsea kwa sasa imeachwa pointi tisa na vinara Manchester City katika msimamo wa Ligi Kuu England na kocha Conte ameanza kuwa na wasiwasi kabla ya kuwavaa Liverpool wikindi ijayo.
Liverpool na Chelsea zote zitacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki hii, lakini vijana wao wa Jurgen Klopp wao watacheza leo Jumanne na Conte na kikosi chake watacheza kesho Jumatano. Chelsea pia watakuwa na safari ya maili 5,800 hadi Baku, Azerbaijan, wakati Liverpool watasafiri kidogo tu hadi Hispania.
Conte anaamini tofauti hiyo ya saa 24 ni kubwa katika maandalizi ya timu yake hasa ukizingatia kwamba, wanasafiri mbali tofouti na wenzao wababe wa Merseyside.
"Jamani aliyeandaa ratiba hii Mungu anamwona,” alisema Conte.
"Ona tuna tatizo la kwanza kwenda kucheza na Qarabag kwao Jumatano na tutarudi huku usiku sana na Jumamosi tuna mechi dhidi ya Liverpool. Kweli hii sawa? Sidhani jamani. Nadhani tuwe tunaangalia jamani kabla ya kupanga ratiba.”