Liverpool yakubali kumsajili Alisson kwa Pauni 67 milioni

Muktasari:

Mpaka sasa haijafahamika ni lini Alisson atatua Liverpool kwa ajili ya vipimo.

Klabu ya Liverpool imekubali kumsajili Kipa wa Roma, Alisson  kwa dau la Pauni 67 milioni.
Uongozi wa Liverpool umejisalimisha kulipa Pauni 58 milioni kisha baadaye watalipa Pauni 9 milioni baada ya kukamilisha mkataba huo.
Mpaka sasa haijafahamika ni lini Alisson atatua Liverpool kwa ajili ya vipimo.
Tangu jana kulikuwa na taarifa kuwa Liverpool inakaribia kumsajili kipa wa Roma, Alisson kwa dau la Pauni 62 milioni kwenye dirisha hili la msimu wa kiangazi.
Kocha Jurgen Klopp tayari alionyesha nia ya kuhitaji huduma ya mlinda mlango huyo ili kumuweka kuwa kipa namba moja kikosini hapo kutokana na Loris Karius kushindwa kumshawishi.
Alisson mwenye miaka 25 amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu msimu uliopita, huku akihakikishiwa mkataba kwenye klabu yake ya Roma.
Kipa huyo raia wa Brazil yupo nchini mwake akiwa mapumzikoni pamoja na familia yake,