Kukosa kombe noma sana! Mourinho agawa medali yake kwa mashabiki

Wednesday August 9 2017

 

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amegawa medali yake kwa mashabiki kutokana na hasira za kufungwa na Real Madrid mabao 2-1.

Kikosi cha Manchester United kilizawadiwa medali pamoja na viongozi wa klabu hiyo, jambo ambalo linadhihirisha kufungwa katika mchezo huo kulivuruga akili ya kocha huyo.

Hata hivyo, Mourinho amejiwekea rekodi ya kocha ambaye hugawa medali zake kwa mashabiki, ambapo akiwa Chelsea mwaka 2006 aliwarushia mashabiki wakati kablu hiyo uilipotwaa ubingwa wa England mwaka huo.