Kocha atetea kidole cha Dele Alli

Saturday September 9 2017

 

LONDON, ENGLAND. Kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino amesema mchekeshaji, Mr. Bean atapaswa afungiwe asionekane kwenye televisheni kama staa wake Dele Alli ataadhibiwa kutokana na kitendo chake cha kuonyesha kidole cha kati.

Dele alifanya tukio hilo katika mechi ya kimataifa kati ya England na Slovakia iliyofanyika Jumatatu iliyopita.
Pochettino amemtetea kiungo wake na kusema huo ni utani aliokuwa akiuelekeza kwa mchezaji mwenzake wa timu ya taifa, Kyle Walker, ambaye walikuwa pamoja Spurs kabla ya beki huyo wa pembeni kuhamia Manchester City kwenye dirisha lililopita. Lakini, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) linadai kwamba Dele alifanya hivyo kumlenga mwamuzi, Mfaransa Clement Turpin na uchunguzi zaidi umeanza kufanyika.