Kocha Klopp ataka taji la EPL msimu huu Liverpool

Muktasari:

Hivyo kocha, huyo amewapa matumaini mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwaeleza kwamba kwa mara ya kwanza katika miaka ya hivi karibuni, timu hiyo inatarajia kutwaa taji hilo.

London, England. Kocha Jurgen Klopp amesema Liverpool inatakiwa kufikiria taji la ubingwa msimu huu walilolikosa kwa takriban miaka 27.

Hivyo kocha, huyo amewapa matumaini mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwaeleza kwamba kwa mara ya kwanza katika miaka ya hivi karibuni, timu hiyo inatarajia kutwaa taji hilo.

Liverpool ilinyakua taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 1990 ikiwa chini ya kocha Kenny Dalglish.

Liverpool inajianda kwa mchezo wake wa kwanza msimu huu ambapo itakutana na Crystal Palace.