Klopp azipa ubingwa klabu za Manchester

Muktasari:

Timu hizo mbili, Man United na Man City zote hakuna iliyopoteza mechi hata moja katika Ligi Kuu England msimu huu ambapo kwa sasa zimeshachezwa mechi tano kwa kila.

KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amekiri Manchester United na Mancheste City ndizo klabu zilizo kwenye hali nzuri kabisa ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
Timu hizo mbili, Man United na Man City zote hakuna iliyopoteza mechi hata moja katika Ligi Kuu England msimu huu ambapo kwa sasa zimeshachezwa mechi tano kwa kila.
Wikiendi iliyopita, Man City ilishusha kipigo kizito cha mabao 6-0 dhidi ya Watford, wakati mahasimu wao wa jijini Manchester, United wao waliichapa Everton 4-0 na kufanya timu hiyo mbili kuwa na pointi sawa, mabao ya kufunga sawa na ya kufungwa sawa kwenye msimamo wa ligi hiyo.