Klopp ajiletea mkosi kwa kumtoa Coutinho

Muktasari:

Klopp amedai kwamba huo ulikuwa ni mpango maalumu kabla ya mechi hiyo na hawakutaka Mbrazil huyo acheze dakika nyingi kwa kuhofia kumchosha zaidi katika mechi zinazofuata.

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp ametetea uamuzi wake wa kumtoa nje kiungo wake mahiri, Phillipe Coutinho katika dakika ya 45 tu ya pambano lao la kombe la Ligi dhidi ya Leicester City juzi ambapo timu yake ilichapwa mabao 2-0 na kutupwa nje ya michuano hiyo.
Klopp amedai kwamba huo ulikuwa ni mpango maalumu kabla ya mechi hiyo na hawakutaka Mbrazil huyo acheze dakika nyingi kwa kuhofia kumchosha zaidi katika mechi zinazofuata.

Ameilaumu safu ya ulinzi ya Liverpool kwa kuzembea na kuruhusu mabao ya Leicester.