Klopp aitambia AS Roma

Muktasari:

Macho ya mashabiki wa soka yatakuwa kwa mshambuliaji wao nyota wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah.

LONDON, ENGLAND. JURGEN Klopp amewaonya wapinzani wao AS Roma huku akitamba Liverpool lazima itaiduwaza dunia kwa kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Macho ya mashabiki wa soka yatakuwa kwa mshambuliaji wao nyota wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah.

Salah amejiunga na Liverpool kutoka AS Roma na amekuwa mchezaji tegemeo akifunga mabao 41 katika mashindano mbalimbali msimu huu.

Kocha huyo amesema ana kikosi imara cha kumpa matokeo mazuri kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa leo usiku.

Klopp amesema Liverpool ina nafasi nzuri ya kuichapa AS Roma ingawa amekiri mchezo utakuwa mgumu.

Mjerumani huyo anasema ataweka historia ya kucheza fainali kama aliyoweka mwaka 2013 akiwa na kikosi cha Borussia

Dortmund. Mara ya mwisho Liverpool kucheza fainali ilikuwa mwaka 2008.

“Huu ni mchezo mkubwa, nimejiandaa kwa mara ya pili kucheza mchezo wa nusu fainali. Kama tutavuka itakuwa mara ya pili

kucheza fainali,” anasema Klopp.