Kipa wa Liverpool ghali zaidi duniani

Muktasari:

Hiyo ni hatua kubwa iliyofanywa kwenye uhamisho wa Liverpool ikiweka rekodi ya kutumia pauni 174.45milioni kwa ajili ya kuwasajili kiungo wa Guinea, Naby Keita, kiungo Mbrazili Fabinho na mshambuliaji Mswisi Xherdan Shaqiri.

Liverpool, England. Alisson amekuwa kipa ghali zaidi katika historia ya soka baada ya Liverpool kukubali kuilipa Roma pauni 65milioni kumnyakuwa Mbrazil huyo.
Hiyo ni hatua kubwa iliyofanywa kwenye uhamisho wa Liverpool ikiweka rekodi ya kutumia pauni 174.45milioni kwa ajili ya kuwasajili kiungo wa Guinea, Naby Keita, kiungo Mbrazili Fabinho na mshambuliaji Mswisi Xherdan Shaqiri.
Alisson aliwasili Merseyside Jumatano na kufanyiwa vipimo vya afya katika hospitali ya Liverpool kwenye uwanja wao wa mazoezi wa Melwood.
Kipa huyo amesaini mkataba wa miaka sita kabla ya kuchukua ndege yake binafsi kurudi Italia kwa lengo la kumalizia mapumziko yake.
Liverpool ilikuwa ya kwanza kuwaomba Roma kuhusu Alisson mwezi Januari, lakini dau lao la pauni 90milioni lilishindikana kutimizwa.
Uhamisho umefanyika wiki hii wakati Chelsea iliyokuwa ikimtaka kuwa katika mipango ya kuuza kipa wao Thibaut Courtois kwa Real Madrid.