Kipa Roma: Hatma yangu itajulikana Russia

Monday June 11 2018

 

By Fadhili Athumani

Rio, Brazil. Kipa wa Brazil, Alisson anaamini hatma yake katika klabu yake ya Roma itaamuliwa kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, Russia.
Kipa huyo, mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake wa sasa na Roma unamalizika 2021, amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kuelekea Santiago Bernabue, Anfield na Stamford Bridge.
Akizungumzia hatma yake mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya Brazil na Austria uliopigwa jana na Brazil kuibuka na ushindi wa goli 3-0, Allison alisema: "Naamini kika kitu kitawekwa bayana kabla ya fainali za Russia."
Aidha, kipa huyo namba wa mabingwa wa kihistotia wa Kombe la Dunia, alisema kama suala halitashughulikiwa mapema kabla ya kuanza kwa kipute hicho, ataamua kupuuzia kila kitu na kuelekeza akili yake katika kuisaidia Brazil.