Kipa Chelsea, Courtois agomea mkataba akidai mshahara zaidi

Muktasari:

Klabu yake, Chelsea ilikuwa na matumaini  ya kuongeza msaada  kwa kipa Thibaut Courtois unaoendelea hadi  2019.

London, England. Kipa namba moja wa Chelsea, Thibaut  Courtois ametikisa kiberiti akitaka mshahara wake wa Pauni 90,000 kwa wiki uongezwe mara mbili.

Klabu yake, Chelsea ilikuwa na matumaini  ya kuongeza msaada  kwa kipa Thibaut Courtois unaoendelea hadi  2019.

Nyota huyo wa  Ubelgiji amekuwa akidai apewe mshahara wa Pauni 200,000  kwa wiki, huku maofisa wa klabu hiyo wakiwa na matumaini kuwa mwafaka utafikiwa ili aendelee kuichezea msimu ujao.

Pande hizo mbili zimekuwa zikiendelea na mazungumzo ambako Courtois  amesema mazungumzo yamesimama kwa sasa.

Nyota mwenzake wa Ubelgiji, Eden Hazard  analipwa Pauni 200,000, sawa na kipa wa Manchester United, David De Gea .

Kocha Antonio Conte  amekuwa na matumaini ya kuendelea kubaki na kipa wake chaguo la kwanza.