Barcelona yamfukuzia kinda Flamengo

Muktasari:

Mchezaji huyo alifanikiwa kufunga mabao matatu kwenye michezo mitatu ya kwanza, jambo ambalo limemfanya kuwindwa zaidi na klabu vigogo barani Ulaya.

Hispania. Klabu ya Barcelona imerudi kwa Flamengo kwa gia nyingine ya kumchukua kinda wake, Lincoln mwenye miaka 16 baada ya kuvutiwa naye kutokana na kiwango alichokionyesha kwenye Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 17.
Mchezaji huyo alifanikiwa kufunga mabao matatu kwenye michezo mitatu ya kwanza, jambo ambalo limemfanya kuwindwa zaidi na klabu vigogo barani Ulaya. Barcelona imeripotiwa kutaka kumsajili Mbazil huyo anayekipiga kwenye klabu ya vijana ya Flamengo.
Tayari Barcelona imeomba kukaa mezani na wawakilishi wa kinda hiyo ili kuzungumzia dau la kumuuza. Mchezaji huyo alisajiliwa na Flamengo  tangu mwishoni mwa mwaka jana.