Kasi ya Rashford, Lukaku kutikisa msimu huu

Hoston, Marekani. Manchester United imewaduwaza majirani zao, Manchester City baada ya kuwafunga mabao 2-0 yaliyofungwa na Romelu Lukaku na Marcus Rashford kwenye mechi ya kirafiki iliyopigwa Houston nchini Marekani.

Lukaku alidhihirisha thamani yake ya Pauni 75 milioni baada ya kufungua pazia la mabao kwenye mchezo huo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu mpya.

Mshambuliaji huyo mpya ameongeza bao la pili ikiwa ni siku tatu tangu afunge bao lake la kwanza walipokutana na Salt Lake City. Naye Rashford hakufanya makosa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan kisha kuujaza mpira wavuni.

Muunganiko wa wachezaji Lukaku, Rashford  pamoja na Paul Pogba unaonekana kuwa tishio katika msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.