Jina laiponza Manchester United

Muktasari:

Manchester United iliipiga Everton mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu wakati Manchester City iliifinyanga Watford mabao 6-0  na kila mmoja kufikisha pointi 13.

England. Ukiangalia msimamo wa Ligi Kuu England, timu mbili hasimu, Manchester City na Manchester United zimefungana kwa kila kitu, lakini jina United ndilo lililoinyima timu hiyo kiti cha Ligi Kuu.
Manchester United iliipiga Everton mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu wakati Manchester City iliifinyanga Watford mabao 6-0  na kila mmoja kufikisha pointi 13.
Baada ya kufungana kwa kila kitu, ikaangaliwa majina ya timu, zote ni Manchester, sasa ikaangaliwa jina la pili, hawa City na wale United.
Kwa United ikala kwao kwa kuwa herufi C inaanza halafu inakuja U kwa hiyo City wanakaa juu kwa herufi yao C.
Sasa ufuatao ni sehemu ya msimamo wa Ligi Kuu kwa timu hizo mbili zilizo juu:

Timu         P    W    D    L    F    A    Pts
1.Man City    5    4    1    0    16    2    13
2.Man United    5    4    1    0    16    2    13