Ivan Perisic akaribia kutua Manchester United

Muktasari:

Mchezaji huyo mwenye miaka 28 anatajwa kutua kwenye dimba la Old Trafford kwa mkataba wa muda mrefu baada ya mipango hiyo kukamilika.

London, England. Winga wa Inter Milan, Ivan Perisic anakaribia kutua mikononi mwa Jose Mourinho ikiwa ni mkakati wake wa kuidaka saini ya mchezaji huyo katika usajili wa kiangazi.

Mchezaji huyo mwenye miaka 28 anatajwa kutua kwenye dimba la Old Trafford kwa mkataba wa muda mrefu baada ya mipango hiyo kukamilika.

Manchester United imeanza vyema mechi zake za kirafiki baada ya kuifunga LA Galaxy mabao 5-2 siku ya Jumamosi wiki iliyopita. Pia leo Jumamne imeifunga Real Salt Lake City mabao 2-1 katika Uwanja wa Rio Tinto kwenye mji wa Utah.