Hatma ya Ronaldo, Messi kuamuliwa usiku wa leo

Muktasari:

Katika fainali 20 zilizofanyika za Kombe la Dunia tangu 1930 ni nchi 77 tu zimeshiriki japo mara moja na timu 12 zimecheza fainali na nchi nane tu zimetwaa ubingwa huo

Moscow, Russia. Kombe la Dunia inajulikani kuwa ni uwanja wa nyota bora duniani kuonyesha uwezo wao, lakini hadi idadi kubwa ya wachezaji hao bado wapo njia panda katika kusaka kufuzu kwa fainali za Russia.
Gareth Bale tayari amejiengua baada ya Wales kutolewa inavyonekana hali hiyo inaweza kuwakumba Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na James Rodriguez ambao bado wanalazimika kufanya kitu katika michezo yao ya mwisho usiku wa leo kujua hatma zao.
Ronaldo kibaruani usiku
Hesabu za Ureno ni rahisi sana wanatakiwa kuifunga Uswisi leo usiku jijini Lisbon na kufuzu kwa fainali za Russia 2018 wakiwa vinara wa kundi. Ila wakifungwa au kutoka sare watalazimika Ronaldo na Ureno yake kusubiri ratiba ya mechi mbili za mtoano zitakazopangwa Novemba kupata tiketi yao.
Messi kujua hatma yake alfajiris
Akiwa amesafiri kwenda Ecuador kwa mchezo wa leo usiku na Argentina, akijua ushindi pekee ndiyo utakawapa nafasi ya kuingia kucheza hatua ya mtoani dhidi ya New Zealand. Endapo watapoteza au kutoka sare jijini Quito itakuwa ni mwisho wa Messi kucheza mashindano hayo makubwa zaidi.
James Rodriguez yuko kwenye hatihati
Colombia ipo Peru kwa ajili ya mchezo wa leo usiku wakiwa na lengo la kuhakikisha wanabaki katika nafasi yao ya nne ili waende Russia. Wakipata Sare itategemea na michezo mingine kupata nafasi ya kucheza hatua ya mtoano, endapo watapoteza itafuta ndoto ya nyota huyo wa Real Madrid kucheza fainali za mwakani.
Alexis Sanchez aivaa Brazil
Wakiwa nafasi ya tatu katika Kundi la CONMEBOL, Chile ipo katika nafasi nzuri ya kufuzu moja kwa moja, lakini kwanza Sanchez anatakiwa kumfunga Brazil jijini Sao Paulo. Wakicheza bila ya uwepo wa Arturo Vidal, mabingwa hao wa Copa America wanahitaji ushindi zaidi ili kujiepusha kugombea nafasi na Argentina.
Luka Modric ndani yamtoano
Katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi Ukraine uliowapeleka Croatia katika mechi za mtoano mwezi ujao, kiungo huyo wa Real, Modric alitegeneza bao la kwanza jijini Kiev. Timu yao ni miongoni mwa nchi nane zitakazosibithishwa Oktoba 16, wakati Fifa itakapotoa viwango vyake na kutangaza makundi ya mechi za mtoano.
Buffon pia anasubiri
Baada ya Hispania kuongoza kundi mbele ya Italia, kipa Gianluigi Buffon sasa anajiandaa kwa mechi za mtoano ili kupata nafasi ya kwenda Russia na kumalizia maisha yake ya soka kwa heshima mwakani.