Iceland kiutani utani watinga Kombe la Dunia

Muktasari:

Timu 17 zimeshakata tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia huku zingine zikipambana na hali zao ili kuhakikisha zinakwenda Urusi mwakani kwenye mashindano hayo yanayoshirikisha timu 32.

Cardiff, Wales. Iceland imeweka historia mpya kufuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Dunia, baada ya kuilaza Kosovo mabao 2-0.
Iceland ndiyo taifa dogo kushiriki fainali hizo. Nchi 17 kati ya 32 tayari zimekata tiketi kucheza fainali hizo zitakazochezwa mwakani nchini Russia.
Mchezaji wa Everton, Gylfi Sigurdsson, alitangulia kufunga bao la kwanza dakika ya 40 kabla ya Johann Gudmundsson kuongeza jingine.