Huyu Del Bosque vipi

HIVI umemsikia yule kocha za zamani wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Hispania, Vicente del Bosque alichosema? Del Bosque haonekani kuiogopa safu hatari ya ushambuliaji ya Liverpool, ambayo kesho Jumamosi itakipiga na Madrid kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayofanyika huko Kiev, Ukraine. Kocha huyo Mhispaniola alisema Salah angeishia tu kukaa benchi kwenye kikosi cha Madrid.

“Real Madrid ni timu bora Ulaya. Sioni kama mchezaji wa Liverpool angepata nafasi mbele ya Bale, Benzema, Cristiano, Asensio na Lucas Vazquez hao wote ni wazuri ya Salah.” Alipoulizwa kuhusu utabiri wake kuhusu matokeo, Del Bosque alisema Liverpool inakufa 4-1.