Huddersfield yafanya usajili wa kwanza kwa kumsajili mshambuliaji wa Porto

Muktasari:

Klabu hiyo, Huddersfield imetangaza usajili na ujio wa mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji akitokea Porto.

Porto, Ureno. Baada ya kupanda daraja, klabu ya Huddersfield imemnasa mshambuliaji wa  Porto, Laurent Depoitre  kwa rekodi yake ya Pauni  3.5 milioni.

Klabu hiyo, Huddersfield imetangaza usajili na ujio wa mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji akitokea Porto.

Akiwa Porto alicheza mechi  10 pekee kutokana na kuumia. Kocha David Wagner  amemsifu Depoitre kuwa mshambuliaji aliyekamilika.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 anafahamika kwa mfumo wake wa uchezaji wa nguvu, amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu hiyo, Terriers.