Hispania wamtimua kocha kuelekea Kombe la Dunia kesho

Wednesday June 13 2018

 

Siku moja baada ya kutangazwa kama kocha mkuu mpya wa Real Madrid, kocha wa timu ya Hispania inayoshiriki fainali za Kombe la Dunia, Julian Lopetegui ametimuliwa kwenye nafasi yake katika timu ya taifa ya nchi hiyo.


Kutimuliwa huko kumekuja saa chache kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Dunia na inatajwa kuwa nafasi yake huenda ikarithiwa na beki wa zamani wa Hispania na Real Madrid, Fernando Hiero.


Fainali za Kombe la Dunia zinatarajiwa kuanza kesho Alhamisi kwa mechi ya ufunguzi baina ya Russia na Saudi Arabia.