Nne Hispania zasubili wabaya wao Ulaya

Muktasari:

Atletico Madrid, Villarreal na Athletic Club zote zitakuwa katika kundi namba moja wakati Real Sociedad ikiwa ni timu pekee itakayokuwa kundi namba mbili.

Madrid, Hispania. Wakati ratiba ya Europa Ligi ikitarajiwa kupangwa kesho, jijini Nyon klabu nne za Hispania zitakuwa zinasubili kuwajua wapinzani wao.
Atletico Madrid, Villarreal na Athletic Club zote zitakuwa katika kundi namba moja wakati Real Sociedad ikiwa ni timu pekee itakayokuwa kundi namba mbili.
Timu hizo zimefanikiwa kuwakwepa miamba mingine katika Kundi namba moja pamoja na Napoli, Borussia Dortmund, Olympique Lyon na Olympique Marseille.
Wakati Real Sociedad ikiwa katika nafasi ya kupangwa dhidi ya CSKA Moscow, Sporting CP, RB Leipzig, AC Milan, Arsenal na Lazio.
Mbali ya timu hizo bado kuna timu nyingine bora zinazowezwa kuwa vikwazo kwa miamba hiyo ya Hispania.
 Italia pia inawawakilishi wanne katika hatua hiyo ya 32 bora wakilingana na Hispania kuwa nchi zenye timu nyingi katika hatua hiyo.
Arsenal kwa sababu imemaliza vinara kwenye kundi lake, haiwezi kupangwa kuchuana na Red Star Belgrade iliyokuwa imepangwa pamoja kwenye Kundi H, jambo linaloifanya kukabiliwa na mechi ngumu zaidi zilizobaki.
Kwenye raundi hiyo ya 32 bora, timu zinazoweza kupangwa dhidi ya Arsenal ni AEK Athens, Borussia Dortmund, Celtic, FC Astana, FC Copenhagen, FCSB Ludogorets, Razgrad, Lyon, Marseille, Napoli, Nice, Ostersunds, Partizan Belgrade, Real Sociedad na Spartak Moscow.
Katika orodha hiyo ya timu, mashabiki wa Arsenal wanaomba wasipangwe na ama Dortmund au Napoli. Kwa sababu Arsenal itakuwa na hadhi, hivyo itaanzia ugenini na mechi ya marudiano itacheza nyumbani.