Herrera apata uhakika wa maisha Manchester United

Muktasari:

Mkataba wa sasa wa Herrera utamalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini United ina nafasi ya kuurefusha kwa mwaka mmoja.

England. Kiungo wa Manchester United, Ander Herrera anatarajiwa kuongeza muda wa mkataba wake katika utiaji saini unaotajwa kufanyika ndani ya miezi miwili ijayo.
Mkataba wa sasa wa Herrera utamalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini United ina nafasi ya kuurefusha kwa mwaka mmoja.
Hata hivyo, Mhispania huyo anaelekea kuwa tayari kukubali mkataba mrefu zaidi baada ya kufanikiwa kuwa na kiwango bora klabu hapo tangu alipowasili mwaka 2014 akitokea Athletic Bilbao.