He! Klopp anajiteteeeea!

Muktasari:

Madai ya kocha huyo wa Liverpool ni kwamba mambo yamebadilika baada ya yeye kufanya usajili ulioweka rekodi kwa kumnasa kipa Alisson kwa Pauni 67 milioni kutoka AS Roma na kumfanya Mbrazili huyo kuwa kipa ghali zaidi duniani.

LIVERPOOL, ENGLAND. JURGEN Klopp ametumia nguvu nyingi kujitetea kwa watu ili asionekane kuwa mbinafsi baada ya miaka miwili iliyopita kuikosoa Manchester United ilipomsajili Paul Pogba kwa pesa nyingi.

Madai ya kocha huyo wa Liverpool ni kwamba mambo yamebadilika baada ya yeye kufanya usajili ulioweka rekodi kwa kumnasa kipa Alisson kwa Pauni 67 milioni kutoka AS Roma na kumfanya Mbrazili huyo kuwa kipa ghali zaidi duniani.

Wakati huo, Klopp alidai hawezi kutoa pesa nyingi kusajili mchezaji mmoja, wakati Man United ilipotumia karibu Pauni 100 milioni kuinasa saini ya Pogba kutoka Liverpool.

Kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, Klopp ameshatumia zaidi ya Pauni 170 milioni kwenye usajili, huku ikiwa ni Januari tu hapo mwaka huu alitoa pesa ndefu kusajili beki wa kati, Virgil van Dijk.

Wachezaji wengine aliowasajili Klopp kwenye dirisha hili ni Naby Keita, Fabinho na Xherdan Shaqiri.

Klopp alisema: “Hii ni soka, sipo kazini tena. Ni kweli, sikuwahi kufikiria kama dunia itabadilika. Pauni 100 milioni ilikuwa pesa nyingi sana, lakini wakati ule dunia imebadilika sana. Sisi sasa tumesajili kipa kwa pesa nyingi zaidi na kumekuwa na usajili mwingine mzuri pia.

“Sio suala la kung’ang’ania mawazo yangu na kuachana kulipa pesa nyingi, kwa sababu kama Liverpool haijafanyikia, yatupasa kufanyika kazi jambo hilo.”

Hadi sasa Klopp ameshatumia Pauni 415 milioni katika kipindi chake cha miaka miwili na nusu tangu alipopewa kazi huko Anfield na wamesubiri kwa miaka sita sasa bila ya taji lolote.