Guardiola kupima mitambo ya ulinzi

Saturday September 9 2017

 

LONDON, ENGLAND. Kocha Jurgen Klopp amesema Philippe Coutinho hatakuwamo kwenye kikosi cha Liverpool kitachomenyana na Manchester City, katika mechi ambayo Pep Guardiola atakuwa kwenye mtihani mzito kutambua kama safu ya ulinzi aliyoisajili itafanya kazi kuwadhibiti washambuliaji kutoka Anfield.
Guardiola na kikosi chake cha Man City leo Jumamosi atakuwa kwenye wakati mgumu huko Etihad kutambua kama kweli pesa nyingi alizotumia kusajili mabeki zinaleta maana wakati akapokabiliana na washambuliaji wenye kasi ya farasi; Mohamed Salah, Sadio Mane, Roberton Firmino na Alex Oxlade-Chamberlain.
Ligi Kuu England inaingia katika wiki yake ya nne, ambapo Man City ambayo imeshinda mara mbili na kutoa sare moja, haina tofauti na wapinzani wao Liverpool, ambao nao wameshinda mechi mbili na sare moja.