Guardiola: Bado muda wa kufikiria ubingwa

Muktasari:

Asema kutokana na kasi ya Manchester United, Spurs sio muda wa kudhani kuwa wanaweza kuwa mabingwa.

London, England. Pep Guardiola amesema ana kazi  ngumu kulinda matokeo mazuri anayopata katika Ligi Kuu England msimu huu, licha ya kuanza vyema msimu huu.
Guardiola ushindi uliopita wa Man City dhidi ya Stoke City mabao 7-2 katika mchezo wa Ligi Kuu isiwe sababu ya wachezaji kubweteka msimu huu.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich, alisema hatarajii kuona ushindi kama huo ukiendelea katika mechi zinazofuata kwa kuwa lolote linaweza kutokea kutokana na ushindani mkali uliopo msimu huu.
“ Lolote linaweza kutokea huu ni mwezi Oktoba. Hatuwezi kutabiri kwamba matokeo kama haya yataendelea kwa msimu mzima. Ni jambo la kujivunia kupata matokeo mazuri lakini bado tuna kazi kubwa mbele yetu,” alisema Guardiola.