Goti lamchelewesha Westbrook kambini

Muktasari:

  • Baada ya upasuaji huo ulioongozwa na daktari wa timu hiyo, Neal ElAttrache kumalizika salama, imeelezwa Westbrook atalazimika kukaa nje wiki nne, huku timu yake ikitarajiwa kuingia kambini wiki mbili zijazo kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

NYOTA na mlinzi matata kabisa wa ligi ya NBA wa Oklahoma City Thunder, Russell Westbrook atalazimika kusubiri kwa wiki mbili kabla ya kujiunga na kambi ya timu yake, baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti la mguu wa kulia wiki hii.

Baada ya upasuaji huo ulioongozwa na daktari wa timu hiyo, Neal ElAttrache kumalizika salama, imeelezwa Westbrook atalazimika kukaa nje wiki nne, huku timu yake ikitarajiwa kuingia kambini wiki mbili zijazo kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Hata hivyo, licha ya upasuaji huo, Westbrook anatarajiwa kuwa fiti kabla ya mchezo wa ufunguzi wa msimu wa kawaida ‘Regular Season’ dhidi ya Golden State Warriors utakaopigwa Oktoba 16. Msimu uliopita, Westbrook aliwaongoza wachezaji wote katika uwiano wa kupika vikapu 10.3 na rebound 10.1 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga triple-double kwa misimu mingi tofauti.