Familia ya Cristiano Ronaldo yahamia Juventus

Muktasari:

Nyota huyo alitambulishwa rasmi juzi Jumatatu kuwa mchezaji wa Juventus kwa mkataba wa miaka minne.

Siku chache kupita baada ya Cristiano Ronaldo kusajiliwa kwa dau la Pauni 100 milioni, nyota huyo ameonekana akiwa na familia yake, huku mwanaye akiwa ametinga jezi ya Juventus.
Nyota huyo alitambulishwa rasmi juzi Jumatatu kuwa mchezaji wa Juventus kwa mkataba wa miaka minne.

Hata hivyo, Juventus na Real Madrid zinatarajiwa kukutana nchini Marekani kwenye mchezo wa kirafiki Agosti 4, huku ikielezwa kuwa Cristiano Ronaldo hatacheza.
Ratiba ya Ligi Kuu Hispania inatarajiwa kutangazwa rasmi Ijumaa wiki hii.
Nyota ahuyo alifunga mabao manne kwenye Kombe la Dunia lililomalizika Jumapili wiki iliyopita kwa Ufaransa kunyakua taji la Kombe la Dunia mwka 2018.