Fabregas amuibukia Messi chumbani

Muktasari:

Chelsea na Barcelona zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali uliochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

London, England.  Cesc Fabregas amevamia vyumba vya kuvalia nguo vya wachezaji wa Barcelona muda mfupi baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kumalizika.

Chelsea na Barcelona zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali uliochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Muda mfupi baada ya mpira kumalizika, Fabregas, alikwenda moja kwa moja ndani ya vyumba vya kuvalia nguo na kuteta na rafiki yake wa muda mrefu Lionel Messi.

Fabregas na Messi walionekana wakifurahia jambo kabla ya kiungo huyo wa Chelsea kupiga picha naye akiungana na kina Andres Iniesta na Luis Suarez.

Wachezaji hao waliwahi kucheza pamoja tangu wakiwa kinda katika kikosi cha Barcelona kabla ya nyota huyo kutimkia Arsenal.

Miamba hiyo inatarajiwa kumenyana katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nou Camp, Hispania Machi 14, mwaka huu.