Everton yamuwashia moto Rooney

Muktasari:

Vipimo vya maofisa wa usalama wa barabarani vilionyesha kwamba Rooney amezidisha ulevi kitu ambacho kilimfanya akutwe na hatia na yeye mwenyewe kukiri kutenda kosa.

WAYNE Rooney amekumbana na adhabu nyingine ukiacha ile ya kuzuiwa kuendeesha magari yake ya kifahari kwa miaka miwili baada ya kupigwa faini ya Pauni 320,000 na klabu yake ya Everton baada ya kukutwa na hatia ya kuendesha gari huku akiwa amelewa na sasa atakuwa anayaangalia kwa macho tu magari yake ya kifahari kwa miaka miwili.
Vipimo vya maofisa wa usalama wa barabarani vilionyesha kwamba Rooney amezidisha ulevi kitu ambacho kilimfanya akutwe na hatia na yeye mwenyewe kukiri kutenda kosa.
Rooney atalazimika pia kufanya kazi kwa saa 100 bila ya malipo kwa kipindi cha miezi 12. Rooney alidakwa akiwa kwenye hali hiyo baada ya kuendeesha gari la mchepuko Laura Simpson kitu ambacho kilitetemesha pia ndoa yake na mrembo Coleen, ambaye ni mama wa watoto watatu. Gari za kifahari za Rooney ni pamoja na BMW i8, Audi Q7, Range Rover Overfinch na Bentley GT.