Duh! Umeisikia hii David Moyes?

Muktasari:

Jinsi ilivyomchinja, hata mwenyewe anashangaa. Ishu ipo hivi, Moyes alikuwa na uhakika wa kupewa muda zaidi wa kuinoa timu hiyo na alipewa mkataba mpya kwenye kikosi hicho cha London.

DUH! West Ham United imemfanyia kitu mbaya sana Kocha David Moyes.

Jinsi ilivyomchinja, hata mwenyewe anashangaa. Ishu ipo hivi, Moyes alikuwa na uhakika wa kupewa muda zaidi wa kuinoa timu hiyo na alipewa mkataba mpya kwenye kikosi hicho cha London.

Lakini, mwenyewe akaremba na kuwaambia mabosi wa West Ham wasubiri msimu umalizike kwanza ndipo waketi chini kujadili malipo yatakavyokuwa, lakini sasa Wagonga Nyundo hao wa London wamemgeuzia kibao na kumtosa kama hawamfahamu vile.

Moyes alitua West Ham United, Novemba mwaka jana wakati alipopewa dili la muda tu kufuatia kuondolewa kwa Kocha Slaven Bilic na alifahamu ataendelea kubaki kwenye timu hiyo, kabla ya mambo kubadilika wiki iliyopita, alipoambiwa hakutakuwa na dili jipya tena hivyo, asepe zake tu.

West Ham sasa imeamua kumpa kazi aliyekuwa kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini na huenda akatua London muda wowote baada ya kuachana na klabu ya Hebei China Fortune aliyekuwa akiinoa huko kwenye Ligi Kuu China.

Chanzo cha habari hiyo kilifichua: “Kila kitu kilikuwa sawa na ilionekana David atabaki. Mabosi walimpa ofa ya kubaki na yeye mwenyewe akasema wasubiri kwanza.”