Dembele aumia, apelekwa Finland

Muktasari:

Barcelona ilitumia Pauni 138 milioni kunasa saini ya mshambuliaji huyo kutoka Borussia Dortmund, lakini akiwa amecheza mechi chache tu, ameumia na hivyo analazimika kwenda kufanyiwa upasuaji.

BARCELONA sasa inalazimika kumtibu staa wake iliyomsajili kwenye pesa nyingi sana, Ousmane Dembele baada ya kuumia misuli ya paja kwenye mechi dhidi ya Getafe.
Barcelona ilitumia Pauni 138 milioni kunasa saini ya mshambuliaji huyo kutoka Borussia Dortmund, lakini akiwa amecheza mechi chache tu, ameumia na hivyo analazimika kwenda kufanyiwa upasuaji.
Bembele alipigwa picha akionekana kwenye kiti cha mataili saa chache kabla ya kusafirishwa kwenda Finland kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo wa kuweka sawa maumivu ya misuli ya paja inayomsumbua.