Totteham yapandisha dau kwa Kane

Muktasari:

Vyanzo vya habari nchini Uingereza, vimedokeza kwamba sababu za kupandisha kwa dau hilo ni kuwadhihirishia kwamba mchezaji huyo hauzwi kwa gharama yoyote.

England. Klabu ya Tottenham imepandisha dau la mshambuliaji wao, Harry Kane hadi kufikia Pauni 200 milioni iwapo Real Madrid ina inataka kumsajili.
Vyanzo vya habari nchini Uingereza, vimedokeza kwamba sababu za kupandisha kwa dau hilo ni kuwadhihirishia kwamba mchezaji huyo hauzwi kwa gharama yoyote.
Dau hilo walilotangaza Tottenham linazidi gharama ya usajili iliyovunja rekodi ya mchezaji wa zamani wa Barcelona aliyehamia PSG, Neymar.