Costa alimwa onyo la mwisho!

Muktasari:

Alisema iwapo ataendelea na tabia hiyo huenda akalazimika kumuacha katika kikosi kitakachoshiriki Kombe la Dunia mwakani.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Julen Lopetegui amemuonya staa wake, Diego Costa kuwa anaihatarisha nafasi yake katika timu ya taifa kama ataendelea na utoro katika kikosi cha Chelsea.
Alisema iwapo ataendelea na tabia hiyo huenda akalazimika kumuacha katika kikosi kitakachoshiriki Kombe la Dunia mwakani.
Costa kwa sasa yupo kwao Brazil akiwa hajacheza hata mechi moja katika kikosi cha Chelsea baada ya kukorofishana na kocha wake, Antonio Conte huku Lopetegui akidai kwamba hatamchagua katika kikosi chake mchezaji ambaye hachezi katika klabu yake.