Conte awapa morali wachezaji ubingwa bado upo kwao

Muktasari:

Conte alisema ingawa Chelsea inakabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi, lakini wachezaji wanatakiwa kupambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha ubingwa unabaki Stamford Bridge kwa mara ya pili mfululizo.

London, England. Kocha wa Chelsea Antonio Conte, amewataka wachezaji wake kuondoa woga katika vita ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
Conte alisema ingawa Chelsea inakabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi, lakini wachezaji wanatakiwa kupambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha ubingwa unabaki Stamford Bridge kwa mara ya pili mfululizo.
Alisema anapitia kipindi kigumu, lakini hatakubali kushindwa na mkakati wake ni kutwaa ubingwa licha ya kukabiliwa na kazi kubwa mbele ya Manchester City, Manchester United na Tottenham Hotspurs zinachuana vikali msimu huu.
Kocha huyo ameingia katika mzozo na Bodi ya Chelsea ambao wameanza kuhoji mwenendo wa timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu England msimu huu.