Christiano Ronaldo arudi na mkosi Madrid ikipigwa bao 1-0

Muktasari:

Kipigo hicho kimemuongezea mawazo kocha Zinedine Zidane kutokana na mchezaji wake, Antonio Sanabria kuwa majeruhi.

Hispania. Mshambuliaji wa Real Madrid, Christiano Ronaldo ni kama amerudi na mkosi baada ya kufungiwa mechi tatu na jana alitinga dimbani wakati timu yake ilipokutana na Real Betis na kupokea kipigo cha bao 1-0.
Kipigo hicho kimemuongezea mawazo kocha Zinedine Zidane kutokana na mchezaji wake, Antonio Sanabria kuwa majeruhi.
Kufungwa kwa Madrid kumewapa nafasi wapinzani wao kuendelea kujiimarisha kileleni kwa tofauti ya pointi saba.