Conte amwaga ugali Chelsea

Saturday January 13 2018

 

London, England. Kocha Antonio Conte amemaliza utata kwa kusema anaweza kuondoka Chelsea mwisho wa msimu huu.
Hatma ya Conte ndani ya Stamford Bridge imekuwa njia panda baada ya kuwepo kwa madai Mtaliano huyo ataachia ngazi mapema.
Kocha huyo wa Chelsea ameshindwa kupiga kwamba anaweza kuacha kibarua hicho kinachompa mshahara wa pauni 9.5 milioni kwa mwaka wakati alipoulizwa kuhusu mstakabali wake wa baadaye.
Alipoulizwa kama ataondoka katika klabu hiyo ya London msimu huu, Conte alisema: "Bado nina mwaka moja katika mkataba wangu hapa, lakini kama unavyojua katika soka lolote linawezekana.
"Wakati furani utakuwa hapa, siku nyingine utakuwa sehemu nyingine."
Alipoulizwa kama ataongeza maktaba wake na Chelsea, Conte aliongeza kusema: "Katika mazingira haya, nafikiri klabu inaweza kuamua kunipeleka sehemu nyingine.
"Kwa kocha wa klabu hii haya ni mazingira ya kawaida, pia kama msimu uliopita ulitwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufika hatua ya fainali ya Kombe la FA. Hiyo ni historia ya klabu kwa kocha wake.